1945 ilikuwa mwaka wa mwisho wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia . Majaribio ya Ujerumani na Japani ya kutawala dunia yalishindwa na mataifa yalitafuta ushirikiano mpya. Ilikuwa pia chanzo cha vita baridi kati ya vikundi wa washindi wa vita kuu baada ya Umoja wa Kisovyeti kujenga utawala wake juu ya nchi za Ulaya ya Mashariki.
Matukio
Waliozaliwa
4 Januari - Richard Schrock , mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia mwaka wa 2005
6 Januari - Philip Schultz , mshairi kutoka Marekani
7 Januari - Raila Odinga , mwanasiasa wa Kenya
20 Januari - Robert Olen Butler , mwandishi kutoka Marekani
6 Februari - Bob Marley , mwanamuziki kutoka Jamaika
9 Februari - Yoshinori Ohsumi , mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba mwaka wa 2016
17 Februari - Elisa David Mollel , mwanasiasa wa Tanzania
20 Februari - George Smoot , mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia mwaka wa 2006
15 Machi - Mohamed Hamisi Missanga , mwanasiasa wa Tanzania
27 Aprili - August Wilson , mwandishi kutoka Marekani
6 Mei - Peter Mahamudu Msolla , mwanasiasa wa Tanzania
8 Mei - Keith Jarrett , mwanamuziki kutoka Marekani
19 Juni - Aung San Suu Kyi , mwanasiasa wa Myanmar na mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani mwaka wa 1991
21 Juni - Aloysius Balina , askofu wa Jimbo Katoliki la Shinyanga , Tanzania
22 Juni - Juma Athumani Kapuya , mwanasiasa wa Tanzania
23 Juni - John Garang , Rais wa kwanza wa Sudan Kusini
30 Julai - Patrick Modiano , mwandishi kutoka Ufaransa na mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi , mwaka wa 2014
31 Julai - Amos Wako , Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Kenya
1 Agosti - Doug Osheroff , mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia mwaka wa 1996
3 Agosti - George Saitoti , mwanasiasa wa Kenya
8 Agosti - Bruno Pius Ngonyani , askofu Mkatoliki nchini Tanzania
17 Agosti - Norbert Wendelin Mtega , askofu Mkatoliki nchini Tanzania
11 Septemba - Franz Beckenbauer , mchezaji mpira na kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani
21 Septemba - Kay Ryan , mshairi kutoka Marekani
18 Oktoba - Huell Howser , mwigizaji wa filamu kutoka Marekani
30 Novemba - Telesphore Mkude , askofu Mkatoliki nchini Tanzania
10 Desemba - Marek Grechuta , mwanamuziki kutoka Poland
bila tarehe
Waliofariki
31 Machi - Hans Fischer , mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia mwaka wa 1930
9 Aprili - Dietrich Bonhoeffer , mwanateolojia nchini Ujerumani , aliuawa na Chama cha Nazi
12 Aprili - Franklin D. Roosevelt , Rais wa Marekani (1933-45)
28 Aprili - Benito Mussolini (kiongozi wa Italia ) anauawa na wanamgambo Waitalia wakomunisti.
30 Aprili - Adolf Hitler (kiongozi wa Ujerumani) anajiua mjini Berlin pamoja na mke wake Eva .
26 Septemba - Bela Bartok , mtungaji wa muziki Mhungaria
19 Oktoba - Hatcher Hughes , mwandishi kutoka Marekani
20 Novemba - Francis William Aston , mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia , mwaka wa 1922
21 Novemba - Ellen Glasgow , mwandishi kutoka Marekani
4 Desemba - Thomas Hunt Morgan , mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba , mwaka wa 1933
9 Desemba - Yun Chi-ho , mwanasiasa kutoka Korea Kusini
Wikimedia Commons ina media kuhusu: