Share to: share facebook share twitter share wa share telegram print page

 

Phiona Mutesi

Phiona Mutesi

Nchi Uganda


Phiona Mutesi (alizaliwa mwaka 1996 hivi[1]) ni mchezaji wa sataranji (chesi) kutoka nchini Uganda.[1]

Phioni ni binti aliyelelewa mjini Kampala katika mtaa wa vibanda wa Katwe. Alipokuwa na umri wa miaka 3 babake aliaga dunia kutokana na ugonjwa wa UKIMWI na muda chache baadaye na dadake alifariki dunia.[1]

Alipofikia umri wa miaka 9 alipaswa kuondoka shuleni kwa sababu mamake hakuweza tena kulipa karo yake. Wakati ule alimsindikiza kakaye kwenda kituo kimoja cha kikristo kilichotoa huduma za michezo pamoja na kuwalisha watoto maskini. Programu mojawapo ilikuwa kundi la sataranji na Phiona asiyeshiriki katika michezo ya uwanjani alichungulia hapa mchezo uliokuwa mpya kwake. Katika muda mfupi alijifunza sataranji na kuonekana mchezaji bora. [1] Alishinda mashindano kadhaa mjini Kampala.

Mwaka 2003 alipelekwa Juba (Sudani) kama mwakilishi wa Uganda katika mashindano ya sataranji ya vijana wa Afrika. Mwaka 2010 alishiriki mara ya kwanza katika olimpiki ya sataranji huko Urusi alipokuwa mchezaji mdogo kabisa kiumri.

Mwezi wa Septemba 2012 alisafiri Istanbul kama mjumbe wa timu ya Uganda akashiriki tena katika olimpiki ya sataranji akaonekana kama mmoja wa wachezaji vijana bora duniani. [2] [2] [3]

Mwaka 2012 kitabu kilitolewa juu ya maisha ya Phiona chenye jina la "The Queen of Katwe: A Story of Life, Chess, and One Extraordinary Girl's Dream of Becoming a Grandmaster", na mwandishi Mwamerika Tim Crothers. [4]

Marejeo

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 "ESPN the Magazine NEXT – Meet chess progidy Phiona Mutesi – ESPN". ESPN. 4 Januari 2011. Iliwekwa mnamo 10 Novemba 2011.
  2. 2.0 2.1 "The chess games of Phiona Mutesi". Chessgames.com. Iliwekwa mnamo 10 Novemba 2011.
  3. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-09-14. Iliwekwa mnamo 2013-01-24.
  4. http://www.amazon.com/The-Queen-Katwe-Extraordinary-Grandmaster/dp/1451657811/ref=sr_1_1?ie=UTF8&qid=1351551869&sr=8-1&keywords=queen+of+katwe

Viungo vya Nje

Kembali kehalaman sebelumnya