Tarehe 1 Januari ni siku ya kwanza ya mwaka . Mpaka uishe zinabaki siku 364 (365 katika miaka mirefu).
Matukio
Waliozaliwa
1431 - Papa Alexander VI
1638 - Go-Sai , mfalme mkuu wa Japani (1654 -1663 )
1909 - Shaaban Robert , mshairi wa Kiswahili kutoka Tanzania
1911 - Audrey Wurdemann , mshairi kutoka Marekani
1941 - Martin Evans , mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba mwaka wa 2007
1941 - Evaristo Marc Chengula , askofu wa Jimbo Katoliki la Mbeya , Tanzania
1950 - Mudhihir Mohamed Mudhihir , mwanasiasa wa Tanzania
1953 - Alpha Blondy , mwanamuziki kutoka Cote d'Ivoire
1954 - Sigfrid Selemani Ng'itu , mwanasiasa wa Tanzania
1960 - Julius Nyaisangah , mtangazaji wa redio kutoka Tanzania
1962 - Richard Roxburgh , mwigizaji wa filamu kutoka Australia
1992 - Jack Wilshere , mchezaji mpira kutoka Uingereza
Waliofariki
Sikukuu
Katika nchi nyingi tarehe 1 Januari ni sikukuu ya Mwaka Mpya
Wakristo wengi, wakifuata mapokeo ya Roma , siku hii ya nane baada ya Krismasi , kwa kukumbuka tohara ya Yesu aliyofanyiwa siku hiyo, huadhimisha sherehe ya Bikira Maria Mama wa Mungu , lakini pia kumbukukumbu za watakatifu Justini wa Chieti , Almaki wa Roma , Eujendo wa Condat , Fuljensi wa Ruspe , Kyaro , Frodobati , Wiliamu wa Dijon , Odilo wa Cluny , Zdislava , Yosefu Maria Tomasi , Vinsenti Maria Strambi , Sigimundi Gorazdowski n.k.
Pia ni siku ya kimataifa ya kuomba amani duniani
Viungo vya nje
WikiMedia Commons
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu . Je, unajua kitu kuhusu 1 Januari kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari .