User:MeAndJesus/sandbox

Askofu Dr. Nathaniel M Kigwila ni Mchungaji kiongozi wa Makanisa ya Growing Mission Church {GMC} na muasisi (founder)wa Huduma ya The Union for the Gospel Ministries {UGM} iliosajiliwa Tanzania na Marekani kwa kufanya kazi ya Mungu.


Askofu Nathaniel M Kigwila ni Mzaliwa wa Tanzania katika mkoa wa Mbeya. Alizaliwa katika mwaka wa 1957 mwezi wa kumi na mbili tarehe 25.


Katika maisha yake amesoma katika shule ya Msingi Majengo Primary school iliopo Mbeya Mjini, katika mwaka wa 1971-1976. Lakini ilipofika Mwaka wa 1977 alianza elimu yake ya Secondary katika shule ya Ruvu/Kibaha iliopo Mkoa wa pwani Tanzania.

Kazi: Aliajiliwa katika kampuni ya TWICO LTD. Dar-Es-salaam. Akiwa karani kisha alipata promotion na kuhamishwa kwenda Dodoma kwa nafasi ya afisa Masoko, mpaka alipoacha kazi rasmi mwaka 1998.

Katika mwaka wa 1990, Mungu alimpa neema ya kwenda Marekani, akiwa ni miongoni mwa Watanzania wachache, ambao walipata nafasi ya kwenda Marekani mapema, pamoja na Mkewe Gloria Lameck, na mtoto wao wa kwanza Abel.

Safari yake ya maisha Marekani ilianza kwa kufikia katika mji wa Birmingham Alabama Cahaba Hights Kisha kuhamia katika mji wa Nashville Tennessee, baada ya muda tena alihamia Charlotte North Carolina, tena baada ya muda pamoja na familia yake walihamia katika mji wa Atlanta Georgia ambapo ndio makazi yake hata Sasa. Pia alikuwa mtanzania wa kwanza kufika Alabama, hivyo aliwapeleka mamia ya watanzania kwa ajili yakusoma, bila kujali kabila, dini, na jinsia. Na mwaka 2022 serikali ya Tanzania ikamtunikia cheti cha uzarendo wa nchi yake.

ELIMU YA JUU YA THEOLOGIA:

• Mwaka 1990-1994 Askofu Nathaniel M Kigwila aliingia kusoma chuo Cha Biblia Birmingham Bible College. (Birmingham Alabama) na kwakupitia chuo hicho alisaidia kupeleka Watanzania wengi sana kusoma.

Na mwaka 1995-1996 aliendelea kusomea elimu yake ya Theologia katika chuo Cha Carver Bible College/equal to Masters, kilichopo Atlanta Georgia. Pia alipitia course mbalimbali za uongozi.

lakini kiu yake na Elimu kumhusu Mungu haikuishia hapo. Mwaka 1998-1999 alisoma katika chuo Cha Brywood Theological Bible School.

Mwaka 2008-2010 akiwa Marekani hukohuko, alisoma katika chuo Cha Theology cha REGAL UNIVERSITY huko North Carolina the Degree of DOCTOR OF DIVINITY.


FAMILIA Ni mume wa Gloria Lameck ambapo wamejaaliwa kupata watoto wanne wa kiume ambao ni Abel, Joel, Hosea na Enoch.


HUDUMA ZA KIJAMII Nathaniel Kigwila ni mtu anaempenda Mungu ambapo alianza kumtumikia tangu akiwa mdogo huko mbeya. Alianza rasmi kusimama madhabahuni akiwa na umri miaka 14 huko Santilia Ilindi Mbeya. Ndie Askofu na muasisi wa kwanza Tanzania kwa kuanzisha Huduma (Ministry) mwaka 1981 hapo Dodoma Huduma iliojulikana kwajina la UNION FOR THE GOSPEL MINISTRIES (UGM) na Makanisa ya Growing Mission Church {GMC} makao makuu yake yakiwa Dar Es Salaam. Na Katika huduma ya Makanisa hayo yanakadiriwa kuwa na matawi mengi katika nchi nzima.

Mbali na huduma ya Makanisa Askofu Nathaniel M Kigwila ni muasisi wa Huduma ya Union for the Gospel Ministries {UGM} huduma iliosajiliwa Tanzania kufanya kazi Ulimwenguni kote ikijikita sana America kwa lengo kubwa la kufanya Mikutano,kwa kuleta wamisionary mbalimbali, nakuendesha Semina na mafundisho ambapo hukutanisha watumishi na waumini wa madhehebu yote katika kujifunza, lakini pia huduma hiyo ya UGM hujikita katika kusaidia watoto yatima ambapo kwa takribani miongo kadhaa huduma hiyo ya UGM chini ya Askofu Nathaniel kigwila na kushirikiana na Wadau mbalimbali na watumishi kutoka Marekani wamekuwa wakitoa misaada kwa watoto hao, kwakulea watoto yatima na walio katika mazingira magumu, walioandikishwa na kutunzwa wako 150. Nathaniel Kigwila amekuwa mtu mweye moyo wa kupenda kusaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu ambapo chini ya maono yake aliweza kusajili taasisi inayofahamika kwa jina la Love and Action (LIA) taasisi hii yenye makao yake Zinga Bagamoyo imejikita katika kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu pamoja na miradi ya viwanda vya chakula kwa lengo la kuuza bidhaa mbalimbali ikiwemo unga ili kusaidia kuendesha taasisi hiyo. Mbali ya LIA kuwa ni taasisi lakini imejikita katika biashara ya uzalishaji wa viwanda mbalimbali ikiwemo utengenezaji wa Unga, Mafuta ya Alizeti pamoja na bidhaa zingine ambapo zaidi ya vijana 160 wamepata ajira.


Mchango katika jamii 12 Desemba 2022: Askofu Nathaniel Kagwila wa makanisa ya Growing Mission Church (GMC) na muasisi wa Huduma ya Union For The Gospel Ministries (UGM) alitunukiwa tuzo ya Uzalendo na Taasisi ya Wananchi Wazalendo Tanzania (TWWT) kufuatia mchango wake mkubwa wa masuala ya kizalendo na taifa lake la Tanzania. Alitunukiwa tuzo hiyo kwenye hafla iliyofanyika katika kanisa lake lililopo Bagamoyo, Pwani nyuma ya shule ya Baobab na kuhudhuriwa na wageni kutoka ndani na nje ya nchi ikiwemo Marekani. Taasisi hiyo iliamuru kumpa tuzo hiyo kwakuwa Mtanzania wa kwanza kusaidia kwanamna Moja au nyingine watanzania zaidi ya 2000 wengi wakiwa wanafunzi kufika Marekani kwa kuwapokea na kuwasaidia kufuata taratibu kama Mtanzania mwenyeji Marekani akiwa amekaa muda mrefu.

Pamoja na kupeleka wanafunzi hao Nchini Marekani pia Bishop Kigwila amefanikiwa kuleta wawekezaki ambao wamewekeza katika Dawa za binadamu kwa kujenga viwanda katika mkoa wa Pwani pamoja na kupeleka dawa hizo katika jeshi la Zanzibar KMKM, Uwekezaji wa kilimo wa viungo mbalimbali unaoendelea katika kijiji cha Mkange Halmashauri ya Chalinze wilaya ya Pwani ulio ajiri Zaidi ya watanzaia 50 pamoja na Kiwanda cha kusaga unga kilichopo eneo la mlingotini Mkoani Pwani, sambamba na hayo Dr Nathanael Kigwila anahudumia Zaidi ya watoto yatima 150 wakishirikiana na wawekezaji na makanisa kutoka nchini Amerika.


BIASHARA Mbali ya utumishi Nathaniel Kigwila ni mfanya biashara katika nchi mbili Marekani na Tanzania. Anajihusisha zaidi na biashara ya mazao mbalimbali pia ni mmiliki wa mashamba katika mikoa ya Pwani,Tanga pamoja na Mbeya ambapo kwa ujumla anamiliki zaidi ya Heka 850 kwajili ya kilimo chini ya kampuni yake ya Kilimanjaro Flavours Company Limited. Kampuni hiyo Hujihusisha zaidi na biashara ya mazao kwa mfumo wa Green House pamoja na mashamba ya kawaida ambayo hulima Mazao ya Parachichi,Nyanya,Mboga Mboga, Pilipili, Hoho, Carrot nk.


Kampuni hiyo imepata mafanikio zaidi kwa kuuza na kusafirisha bidhaa hizo nje ya nchi kwa nchi kama vile Germany, Dubai,Uturuki na nchi kadhaa za Ulaya na Uarabuni.


Utajili: Anakadiriwa kuwa na utajiri wenye thamani ya Dollar za kimarekani zaidi ya $10M. Utajiri huo unatokana na vyanzo mbalimbali ikiwemo Biashara, Kampuni, Makanisa, na Mali binafsi kama vile Nyumba, Magari na vitu vingine.


reference mbalimbali


https://fullshangweblog.co.tz/2022/11/13/mtanzania-mzalendo-aliyewapeleka-zaidi-ya-watanzania-2000-marekani-kutunukiwa-cheti-cha-heshima/


https://globalpublishers.co.tz/askofu-kigwila-atunukiwa-cheti-cha-uzalendo/

Content Disclaimer

Informasi ini disarikan dari Wikipedia dan disajikan kembali untuk tujuan edukasi. Konten tersedia di bawah lisensi CC BY-SA 3.0. Kami tidak bertanggung jawab atas ketidakakuratan data yang bersumber dari kontribusi publik tersebut.

  1. The information displayed on this website is sourced in part or in whole from Wikipedia and has been adapted for the purpose of restating it. We strive to provide accurate and relevant information, however:
  2. There is no guarantee of absolute accuracy. Wikipedia is an open, collaborative project that can be edited by anyone, so information is subject to change.
  3. It is not intended to constitute professional advice. The content displayed is for informational and educational purposes only. For important decisions (e.g., medical, legal, or financial), please consult a professional.
  4. Content copyright. Wikipedia is licensed under the Creative Commons Attribution-ShareAlike License (CC BY-SA). This means that content may be reused with appropriate attribution and shared under a similar license.
  5. Responsible use. Any risk arising from the use of information from this website is entirely the responsibility of the user.