Mikoa hiyo yote imegawanyika tena kwenye wilaya 169. Wilaya zimeganyika katika kata kibao.
Historia ya mikoa
Ugawaji wa nchi wakati wa ukoloni
Utawala wa Kijerumani
Wakati wa ukoloniwa Kijerumani eneo la Tanzania Bara (=Tanganyika) lilikuwa pamoja na Rwanda na Burundi kama Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Mwaka1913 eneo lote liligawiwa kwa mikoa 21 na maeneo matatu ya wawakilishi wakazi. Mikoa 19 ilikuwa chini ya wakuu wa mkoa wa kawaida yaani maafisa raia Wajerumani (jer.Bezirksleiter au Bezirkamtsmann) waliyemwakilisha gavana na mikoa miwili ilikuwa chini ya mamlaka ya kijeshi yaani afisa wa jeshi la kikoloni la schutztruppe.
Mikoa miwili ya Iringa na Mahenge ilikuwa "mikoa ya kijeshi" yaani chini ya usimamizi ya maafisa wakuu wa jeshi la Schutztruppe.
Maeneo ya Bukoba (takriban sawa na Mkoa wa Kagera wa leo), Ruanda na Urundi yaliendelea kutawaliwa na watawala wao wa kienyeji wakiangaliwa na mwakilishi mkazi wa Ujerumani aliyekuwa kama balozi, mshauri mkuu na msimamizi wa watawala hao.
Utawala wa Kiingereza
Tangu mwaka 1918/1919 eneo la Tanganyika lilikuwa eneo la kudhaminiwa kwa Uingereza bila maeneo ya Rwanda (Ruanda) na Burundi (Urundi). Tanganyika ikigawiwa mwaka 1922 kuwa na mikoa ileile ilhali majina ya Kijerumani yalibadilishwa kuwa majina ya kienyeji kama vile [2]:
Mwaka 1967 Zanzibar Shambani (Rural) ikagawiwa kuwa Zanzibar Shambani Kaskazini na Zanzibar Shambani Kusini. Mikoa hiyo iliitwa baadaye Kaskazini Zanzibar na Kusini Zanzibar.
1971 Mkoa wa Rukwa ulianzishwa kutokana na maeneo ya Mbeya na Tabora.
1972 Mkoa wa Lindi ukatengwa na Mtwara.
1974 Mkoa wa Dar es Salaam ukatengwa na Mkoa wa Pwani
1982 Mkoa wa Pemba ukagawiwa kuwa Kaskazini Pemba na Kusini Pemba
1984 Jina la Mkoa wa Ziwa Magharibi likabadilishwa kuwa Mkoa wa Kagera
2002 Mkoa wa Manyara ukatengwa na Arusha,
Mwaka 2012 mikoa minne mipya ilianzishwa ambayo ni
Mkoa wa Geita, kutoka maeneo ya mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Kagera
Mkoa wa Katavi, awali ilikuwa Wilaya ya Mpanda katika Mkoa wa Rukwa
Mkoa wa Njombe, kutoka maeneo ya Mkoa wa Iringa (wilaya za Ludewa, Makete na Njombe)
Mkoa wa Simiyu, kutoka maeneo ya mikoa ya Shinyanga (Bariadi, Meatu na Maswa) na Mwanza (Busega).
Mwaka 2016 ulianzishwa mkoa wa Songwe kwa kumega mkoa wa Mbeya upande wa magharibi.
Makala hii kuhusu maeneo ya Tanzania bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mikoa ya Tanzania kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.