Hidrojeni
Hidrojeni (ing. hydrogen) ni elementi ya kikemia yenye namba atomia 1 na uzani wa atomi 1.00794. Alama yake ni H. Ni atomi nyepesi kati ya elementi zote hivyo ina nafasi ya kwanza katika mfumo radidia Hidrojeni ni elementi inayopatikana kwa wingi kabisa ulimwenguni lakini si duniani. Iko ndani ya maji na katika molekuli zote za mada hai. Muundo wa atomiAtomi za H zina elektroni moja tu inayozunguka kiini cha atomi. Hidrojeni ya kawaida ina protoni moja tu. Hii ni zaidi ya asilimia 98 ya isotopi zote za hidrojeni. Kuna pia isotopi yenye nyutroni moja au mbili katika kiini lakini zinatokea mara chache tu. Kuna isotopi mbili zinazoitwa Duteri (deuterium) na Triti (tritium). Kupatikana kwake ulimwenguniDuniani kwa kawaida hakuna hidrojeni ya atomi moja moja hutokea kama gesi yenye molekuli za H2. Masi ya jua letu ni hasa hidrojeni lakini pia sehemu kubwa ya masi za sayari kubwa yaani Mshtarii, Zohali, Uranus na Neptun. Kwa jumla asilimia 93 za atomi zote na asilimia ya masi katika mfumo wa jua letu ni H.
|